top of page
Search

"A smile is better shared"

  • Nov 18, 2024
  • 2 min read

Updated: Jan 10

Ukiwa umekaa na watu ukatabasamu na wao wasijue kipi kimekufanya utabasamu basi watahisi unawacheka. PDT tumeliona hilo ndiomana tumetenga rasimali za muda na fedha kuhakikisha tabasamu zetu sio zetu tu bali ni za wengi.

Salamu za upendo kwa wadau wetu wote!


SHUKRANI ZETU KWAKO


Leo tunapenda kushiriki tabasamu zetu za dhati na shukrani za moyoni kwa kila mmoja wenu aliyeguswa na kuamua kugusa maisha ya wengine. Kila michango yenu, ndogo au kubwa, imekuwa taa ya matumaini kwa watoto wenye uhitaji.


Tabasamu yetu leo si ya siri – ni ishara ya furaha na shukrani tunayoishiriki na jamii nzima. Tunatambua kuwa kila mchango ni ishara ya imani yenu katika ndoto yetu ya pamoja ya kujenga jamii bora.


WITO WETU MPYA: "NISHIKE MKONO, NIRUDI SHULENI"



Leo, tunazindua kampeni mpya yenye lengo la kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki nyuma katika safari ya elimu. Kampeni yetu "Nishike Mkono, Nirudi Shuleni" ni wito wa dharura kwa jamii nzima:


• Tunahitaji kushikana mikono

• Tunahitaji kuunganisha nguvu

• Tunahitaji kila mmoja wetu kuwa sehemu ya suluhisho


Ukweli unatuuma – maisha ya sasa yamekuwa ya kujitenga na jamii, hasa wale walio na uhitaji mkubwa. Watoto wetu wanahitaji zaidi ya msaada wa kifedha – wanahitaji mioyo yetu, wanahitaji mikono yetu kuwashika na kuwaongoza.


TUUNGANE PAMOJA


Kwa kila mtoto anayehitaji kurudi shuleni, kuna nafasi ya mtu kama wewe kuwa mwanga wake wa matumaini. Tunawakaribisha tena:


1. Kuchangia kwa hali na mali

2. Kushiriki ujumbe wetu

3. Kuwa balozi wa kampeni hii

4. Kutambua watoto wanaohitaji msaada katika jamii yako


Kumbuka, tabasamu yako leo inaweza kuwa chanzo cha matumaini kwa mtoto kesho. Tushikane mikono, tuwarudishe watoto wetu shuleni.

Kujua Zaidi Piga
0764044558
Michango
MPESA LIPA: 54363609 JINA: PASSION OF DEVELOPMENT FOR TRANSFORMATION NMB TZS: 20110093578 NMB USD: 20110093579 JINA: PASSION OF DEVELOPMENT FOR TRANSFORMATION

Asanteni.


Tazama Picha za tukio lilopita hapa



Matukio katika picha Kisarawe
A smile is better Shared





PDT Event at Kisarawe
A smile is better shared



PDT Event at Kisarawe
Upendo, Umoja, Kujitoa

Picha ya pamoja kilele cha kampeni ya "A smile is better shared" na PDT
A smile is better shared

PDT Event
A smile is better shared

 
 
 

Comments


bottom of page